Jaji wa shirikisho ametupilia mbali mashtaka ya uhalifu wa kimfumo (RICO) dhidi ya Sean Diddy” Combs katika kesi iliyofunguliwa na Rodney “LiRod” Jones, mshirika wake wa zamani.
Hata hivyo, mahakama imeamua kuwa madai ya unyanyasaji wa kijinsia na usafirishaji wa binadamu kwa ajili ya ngono yana msingi wa kuendelea kusikilizwa mahakamani, Kulingana na uamuzi wa jaji, madai ya RICO hayakuwa na uhusiano wa moja kwa moja na malipo ambayo Jones anadai hakupata kutokana na kazi yake kwenye albamu ya Love ya Diddy.
Licha ya mafanikio hayo kwa upande wa Diddy, mashtaka makubwa ya unyanyasaji wa kijinsia bado yanabaki kuwa changamoto kubwa kwake, huku kesi hiyo sasa ikielekea mahakamani kwa usikilizaji zaidi.
Diddy ameendelea kukanusha tuhuma zote dhidi yake Kesi hii inazidi kuzua mijadala mikali, ikitokea wakati ambapo wasanii wengi wa hip-hop wanakumbwa na mashtaka yanayohusiana na unyanyasaji wa kijinsia na matumizi mabaya ya mamlaka,