
Diddy anatuhumiwa kumlazimisha mtoto wa miaka 10 kufanya kitendo cha kingono ili kupata nafasi ya kuwa staa. Tuhuma hizi zimeibuliwa kwenye kesi mpya iliyowasilishwa Jumatatu na mlalamikaji anayetajwa kama John Doe.
Kwa mujibu wa nyaraka zilizoibuliwa na TMZ, kijana huyo anadai kuwa mwaka 2005 alienda New York City na wazazi wake kwa ajili ya kuonana na Diddy kwa majaribio ya muziki.
Anadai kwamba walipokutana, Diddy alimwambia kuwa anaweza kumsaidia kufanikiwa kuwa staa, lakini lazima atoe uthibitisho wa kuhitaji nafasi hiyo kwa gharama yoyote.
Mlalamikaji anadai alipewa soda ambayo alihisi kuwa na kilevi baada ya kunywa. Baadaye, alidaiwa kulazimishwa na Diddy kufanya kitendo kisicho cha hiari kisha alipoteza fahamu, na alipokuja kuzinduka alikuta nguo zake zikiwa zimefunuliwa.
Wakili wa Diddy alikanusha madai hayo kwa kusema kwamba ni juhudi za kutafuta kiki, na kwamba wana uhakika mchakato wa kisheria utathibitisha kuwa Diddy hakuwahi kumdhuru yeyote kingono.

