KENYA-Kiongozi wa Muungano wa Azimio la Umoja, #RailaOdinga amemjibu Balozi wa Marekani Nchini humo, Meghan
Whitman, kuwa #Kenya sio koloni la Marekani na kumtaka kujiepusha na Siasa za Kenya, la si hivyo Watafanya mazungumzo ili arudishwe Marekani.
Hii ni siku mbili baada ya Whitman kusema Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2022 ulikuwa Huru na wa Haki na Rais #WilliamRuto alimshinda Odinga kwa njia ya Haki Akizungumza katika Mkutano uliofanyika Eldoret amesema,
“Mwishowe, nataka kumwambia Balozi, acha Wakenya waendelee na mambo yao, ikiwa Maandamano yanaweza kuleta mazungumzo
kati ya Serikali na Upinzani basi kila kitu kiko sawa na Maandamano. Mwambie Balozi huyu Kenya sio Marekani, Kenya sio Koloni la
Marekani, funga Mdomo wako ukiwa hapa au tutakurudisha Nchini kwako.”