Site icon Bongo Plus

Rais Samia Amteue Tena Majaaliwa Waziri Mkuu

Mbunge wa Jimbo la Manonga Mkoani Tabora Seif Khamis Gulamali ameitaka Serikali kutosita kuchukua mikopo kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo nchini Tanzania, akieleza kuwa deni la Taifa ambalo
limetajwa kuwa ni Tsh. trilioni 97 bado ni himilivu na la chini kulinganisha na Mataifa mengine ya Afrika mashariki.

Gulamali amesema hayo jana Alhamisi April 10, 2025 wakati akichangia maoni yake kuhusu Hotuba ya Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka 2025/26, akimsifu
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kwa usimamizi mzuri wa shughuli za Serikali tangu kuteuliwa kwake kuwa Waziri
Mkuu, miaka kumi iliyopita.

Gulamali amesema ziara mbalimbali za Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ikiwemo ziara yake ya hivi karibuni aliyoifanya Wilayani lgunga Mkoani Tabora imekuwa na neema kwa Wananchi, akimuomba Rais Samia Suluhu Hassan kuendelea nae kama Waziri Mkuu mara baada ya uchaguzi wa Oktober 2025.

Exit mobile version