Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluh Hassan leo Jumamosi Machi 08, 2025, amewasili Mkoani Arusha kupitia uwanja wa ndege wa Kimataifa
KIA, na kupokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe.
Paul Christian Makonda na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Nurdin Babu na Viongozi wengine wa Chama Cha Mapinduzi na serikali. Rais yupo Mkoani Arusha kuongoza maadhimisho ya siku ya wanawake kitaifa katika viwanja vya Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha.