Mheshimiwa Ruto atapokelewa kwa gwaride la heshima na mwenyeji wake, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, Ikulu Dar es Salaam ambapo pia watafanya mazungumzo ya uwili ili kuimarisha uhusiano wa Tanzania na Kenya.
Mapema kesho, Mei 5, 2026, Mheshimiwa Ruto atalihutubia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jijini Dodoma kabla ya kuhitimisha ziara yake
