Site icon Bongo Plus

Rais wa Marekani Biden Kuzuru Israel Kufanya Mazungumzo na Netanyahu.

 

Rais wa Marekani Joe Biden anatarajiwa kufanya ziara nchini Israel siku ya Jumatano, ambapo atakutana na kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa nchi hiyo Benjamin Netanyahu.

Katika mazungumzo yao, Biden anatarajiwa kuithibitishia nchi hiyo juu ya uungaji mkono katika kuhakikisha usalama wa lsrael.

DW imeripoti kuwa ziara hiyo ya Biden nchini humo, imetangazwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken leo Jumanne.

Blinken amesema Rais Biden atathibitisha tena uungwaji mkono thabiti wa Marekani kwa Israel na
kujitolea kwa nchi hiyo kwa ajili ya usalama wa Israel.

Blinken ameongeza kuwa lsrael ina haki na wajibu wa kuwalinda raia wake dhidi ya Hamas na makundi mengine ya kigaidi na kuzuia mashambulizi ya siku
za usoni.

Akizungumza na waandishi habari, Blinken amesema, amekubaliana na Waziri Mkuu Netanyahu kuhusu mpango utakaowezesha misaada ya
kibinadamu kuwafikia raia ndani ya Gaza.

Exit mobile version