Site icon Bongo Plus

Rais wa Rwanda Paul Kagame ameanzisha safari zisizohitaji visa kwa Waafrika wote

Rais wa Rwanda Paul Kagame ameanzisha safari zisizohitaji visa kwa Waafrika wote, na kuifanya Rwanda kuwa nchi ya nne barani Afrika kufanya hivyo.

“Tumeondoa vizuizi vya visa kwa raia wa kila nchi ya Afrika pamoja na mataifa mengine, Mwafrika yeyote anaweza kupanda ndege hadi Rwanda wakati wowote anaotaka na hatalipa chochote kuingia nchini mwetu” Rais Kagame.

Rwanda sasa inaungana na Ushelisheli, Gambia na Benin, zikiwa ni nchi pekee za Kiafrika zinazotoa visa bila malipo kwa raia wote wa Afrika.

Hata hivyo Rwanda imekuwa kwenye kampeni ya kukuza sekta yake ya utalii, ikishirikiana na vilabu vya soka kama Arsenal na Bayern Munich ili kuitangaza nchi hiyo kama kivutio cha watalii.

 

Exit mobile version