shirika la @nic_insurance leo limetimiza miaka 60 tangu kuanzishwa kwakwe kutoa huduma za bima kwa Watanzania.
Kama washirika wa NIC Insurance, Klabu ya Young Africans imeungana nao kusherehekea kilele cha miaka hii ya kumbukumbu.
Kwa niaba ya Uongozi wa Young Africans, Bwana Andre Mtine, Mkurugenzi Mtendaji wetu amekabidhi zawadi ya keki na jezi iliyosainiwa na Wachezaji wetu kwa NIC Insurance kama ishara ya kuenzi siku hii muhimu katika historia yao🔰

