Site icon Bongo Plus

Simba Kugharamia Uharibifu Uliotokea Benjamin Mkapa

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo, Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi amemuagiza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo kuchukua hatua mara moja kwa kuwaandikia timu ya Simba SC na kuwanakili Shirikisho la Mpira Tanzania (TFF) ili gharama za uharibifu uliotokea wakati mechi ya Kombe la Shirikisho Afrika hatua ya makundi kati ya Simba SC dhidi ya SC Sfaxien zilipwe.

Katika taarifa iliyotolewa na Wizara hiyo imeeleza kuwa wizara imesikitishvwa na vitendo vya mashabiki kung’oa na kuharibu viti vya kukalia watazamaji katika Uwanja wa
Benjamin Mkapa, jijini Dar es Salaam katika mchezo huo ambao ulipigwa jana Desemba 15, 2024 kuanzia majira ya saa 10:00 jioni.

“Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mheshimiwa Prof. Palamagamba Kabudi amemuagiza Katibu Mkuu wa Wizara kuchukua hatua mara moja kwa kuwaandikia timu ya Simba SC na kuwanakili TFF ili
gharama za uharibifu uliosababishwa wakati mechi hiyo zilipwe” taarifa ya Wizara.

Aidha Prof. Kabudi amewataka mashabiki wanaoingia katika Uwanja wa Benjamin Mkapa kuacha vitendo vya uharibifu wa uwanja kwa kuwa wanasababisha hasara
kwa Serikali na kuharibu ubora wa uwanja.

“Vitendo vilivyofanyika jana katika Uwanja wa Benjamin Mkapa havikubaliki na sio vya kimichezo, nakuelekeza Katibu Mkuu kuchukua hatua mara moja.

“Pamoja na kuwaandikia Simba Sports Club na TFF, wapeni ushirikiano Polisi ili watu wote waliokuwa wanang’oa viti na kuvitupa wakamatwe na wachukuliwe hatua za kisheria, lazima tabia hii ikomeshwe” amesema Prof. Kabudi

Exit mobile version