Site icon Bongo Plus

Treni Zagongana Wingereza 89 Wajeruhiwa

Dereva mmoja wa treni amefariki dunia huku Watu 89 wakijeruhiwa baada ya treni mbili za abiria za Kampuni ya East Midlands Railway kugongana Kusini mwa Mji wa Bedford, karibu kilomita 100 Kaskazini mwa London, Uingereza.

Ajali hiyo ilitokea jioni ya ljumaa Juni 19, 2026 wakati treni hizo zilipokuwa zikielekea Kituo cha St. Pancras Jijini London.

Kwa mujibu wa Polisi wa Usafiri wa Uingereza, tukio hilo limetangazwa kuwa ajali kubwa huku Vikosi vya Dharura vikijumuisha zaidi ya magari 20 ya wagonjwa, helikopta sita za matibabu pamoja na vikosi vya zimamoto vikipelekwa eneo la tukio.

Mamlaka za Afya zimesema Watu 11 walipata majeraha mabaya, 22 walijeruhiwa na wengine 56 walipata majeraha madogo. Baadhi ya manusura wamesema walirushwa kwa nguvu kutoka kwenye viti vyao baada ya treni hizo kugongana, huku wakishuhudia wenzao wakivuja damu na wengine wakivunjika mifupa.

Chama cha Wafanyakazi wa Reli, Bahari na Usafirishaji Nchini Uingereza (RMT) kimethibitisha kuwa aliyefariki ni dereva wa mojawapo ya treni hizo na alikuwa mwakilishi wa zamani wa chama hicho, huku uchunguzi ukiendelea kubaini chanzo cha ajali hiyo.

Exit mobile version