Site icon Bongo Plus

Trump Anaswa Akisinzia Kwenye Kikao na Mawaziri

Rais wa Marekani, Donald Trump, amezua gumzo baada ya kuonekana kana kwamba anasinzia wakati wa kikao cha Baraza la Mawaziri kilichofanyika Jumanne Ikulu ya White House. Katika tukio lililodumu saa mbili na dakika 18, kamera zilimnasa rais huyo mwenye umri wa miaka 79 akifumba macho mara kadhaa na kuonekana kukabwa na usingizi wakati mawaziri wake wakitoa taarifa na sifa kuhusu kazi zao.

Tukio hilo limeibua mjadala mpya kuhusu umri wake na uwezo wa kushughulikia majukumu mazito ya urais, hasa baada ya vyombo vya habari kuripoti kuwa huenda anahisi athari za uzee akiwa madarakani, mada ambayo Trump mwenyewe ameipinga vikali, akisema ni upotoshaji wa vyombo vya habari.

Hata hivyo, kwa mujibu wa video na mashahidi wa ndani, nyakati za kusinzia ziliendelea kujirudia wakati kikao kikiendelea, jambo lililoongeza mjadala mpana mtandaoni kuhusu afya na umakini wa rais huyo katika majukumu ya kila siku.

Exit mobile version