Site icon Bongo Plus

Trump Asitisha Msaada wa Kijeshi Ukraine

Rais wa Marekani Donald Trump amesimamisha msaada vwa kijeshi kwa Ukraine hatua ambayo inajiri siku chache tu baada ya makabiliano ya hadharani kati ya Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky na Trump Ikulu ya White House.

Trump mapema Jumatatu alikuwa amekataa kufuta uwezekano wa kusitisha msaada huo wakati alipoulizwa na waandishi lakini usitishwaji woWote Wwa silaha za Marekani kwenye uwanja wa mapambano utadhoofisha pakubwa nafasi ya Ukraine kuukabili uvamizi wa Urusi, Afisa mmoja wa lkulu ya White House amesema Trump amekuwa wazi kuwa lengo lake ni amani.

Gazeti la New York Times limeripoti kuwa kusitishwa huko kumeanza kutekelezwa mara moja na kutaathiri silaza zenye thamani ya mamia ya mamilioni ya dola zilizopaswa kupelekwa Ukraine, Zelensky Jumatatu alisema kuwa anataka vita hivyo vimalizike haraka iwezekanavyo.

Exit mobile version