Site icon Bongo Plus

“Tumezuiliwa Kufanya Mkutano lla Tutarudi Tena” Heche

Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Tanzania Bara, John Heche, amesema licha ya jeshi la Polisi kuzuia mkutano wao ambao ulipangwa kufanyika Mbarali Mkoani Mbeya leo March 25, 2025 watarudi tena na kufanya mkutano katika eneo hilo.

Heche amesema hayo baada ya Jeshi la Polisi kuwazuia kufanya mkutano wa ndani pamoja na mkutano wa hadhara katika eneo la Mbarali wakiwaeleza kuwa barua yao inaonesha walitakiwa kufanya mikutano hiyo March 24 na sio March 25 kama ambavyo wao walitaka kufanya.

Amesema ni kweli awali barua ya Chama hicho ilikosewa tarehe lakini licha ya kumuomba na kukubaliwa na Mkuu wa Polisi Wilaya ya Mbarali na kutakiwa kuandika barua ya kurekebisha tarehe ya mikutano yao lakini wameshangaa leo Jeshi la Polisi limewazuia kufanya hata mkutano wa ndani huku wakimzuia Heche hata kushuka kwenye gari lake

“Sababu zao ni zilezile ambazo hazina msingi sana wanasema barua yetu ilikosewa lakini wamezuia mpaka mkutano wa ndani ambao kisheria hauitaji kuandika barua kwahiyo ni hofu kujaribu kuhujumu no reforms no election, wala hatuna wasiwasi tutaendelea na mapambano tumesalimia Wananchi tumewaomba kwamba tutazungumza nao tarehe 31 tutarudi hapo kufanya mkutano”

Exit mobile version