Site icon Bongo Plus

Uganda Yazuia Shambulio la Bomu Waliopanga Kulipia Kanisa.

Rais Yoweri Museveni amesema, Polisi wa Uganda walitibua shambulio la bomu dhidi ya Makanisa lililopangwa na kundi la waasi la Allied
Democratic Forces (ADF) katikati mwa Wilaya ya Butambala.

Wanamgambo hao wanaohusishwa na Islamic State siku ya Jumapili, Oktoba 15 walipanga kutega mabomu mawili katika Makanisa ya Kibibi, karibu
kilomita 50 kutoka mji mkuu Kampala.

Mapema siku hiyo hiyo, Museveni alisema vikosi vya Uganda vilifanya mashambulizi ya anga dhidi ya ngome nne za ADF katika nchi jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Alionya kwamba ADF wanaotoroka “wanaingia tena Uganda na kujaribu kufanya vitendo vya kigaidi vya
kubahatisha”.

Mwezi Juni, wanamgambo wa ADF waliwaua watu 42, wakiwemo wanafunzi 37 katika shule ya Sekondari, Magharibi mwa Uganda karibu na mpaka na DR Congo, moja ya mashambulizi mabaya zaidi ya ADF nchini humo.

Exit mobile version