Site icon Bongo Plus

Ujumbe wa Breezy Baada ya Ushindi wa Grammy Awards 2025

Baada ya kutwaa tuzo ya Grammy ambayo aliikosa kwa zaidi ya miaka 10, Chris Brown ame-share ujumbe mzito kwa mashabiki zake kupitia ukurasa wake wa instagram akieleza namna ambavyo hajaichukulia poa support yao.

“Asante Mungu kwa kunifunika kwa upendo wako na asante mashabiki wa Breezy kwa kuwa na mimi kwa kila hali, asante kwa watoto wangu! asante kwa kila mtayarishaji, mwandishi, Uongozi,RCA, timu za mitaani,redio,wapiga picha, wakurugenzi na shukrani kwa Grammy.

Hii ni mara ya pili kwa Breezy kushinda tuzo ya Grammy ambapo tarehe 12 February 2012 alifanikiwa kushinda tuzo ya Albamu Bora ya R&B kupitia “FAME”.

Exit mobile version