Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu amewataka Watanzania wakiwemo Viongozi wa Dini kuwa na ustahimilivu na kutoivuruga amani ya nchi huku akisema hata kama Mtu hampendi yeye Dkt. Samia avumilie asubiri amalize muda wake badala ya kuchochea kuvuruga amani ya nchi.
Akiongea na Wazee wa Dar es salaam leo December 02, 2025, Rais Samia amesema “Hata kama aliyopo juu ya Serikali haumtaki, kuna muda, hii nchi ya kidemokrasia huyu Mtu ataongoza hadi kipindi hiki kafanya kosa semeni, kosa la Serikali ya awamu ya sita kuongeza huduma za afya bora kwa Watanzania na mashule mazuri?, kosa letu kukuza uchumi wa Tanzania hadi ukasifiwa Duniani?” kosa letu ni nini?, kama Mtu hampendi anayeongoza tustahimili tu, ataongoza ataondoka, kwani wote walioongoza tangu awamu ya kwanza wote walipendwa?, kwani kulikuwa na vurugu?, kama haumpendi Samia kisa Dini yake au alikotoka hakuna sababu ya kuvuruga nchi”
“Niwaombe sana zile sumu zinazotiwa huko, mnapotiwa sumu tumieni akili zenu, najua hakuna eneo baya la kumpata Mtu kama Dini, ukimkamata Mtu kwenye Dini na ukamlisha ubaya unajenga chuki ndani ya moyo, Wanasiasa wanamuharibu Mtu kichwani”
“Kwahiyo Viongozi wa Dini kaeni kwenye mstari wenu, Dini zetu zote zinasema kila Mamlaka imeletwa na Mungu, iwe kwenye Mamlaka kuna Mwanamke au Mwanaume zimeletwa na Mungu, Mungu ndio anajua kwanini Samia yupo hapa, Viongozi wa Dini majoho yetu yaoneshe sura halisi, hakuna kitabu cha Dini kimesema kitatumia Dini kuvuruga nchi, niwaombe Viongozo wa Dini tusivuruge nchi yetu”

