Jarida la Forbes limeripoti kuwa Elon Musk ameendelea kushikilia nafasi ya mtu tajiri zaidi duniani baada ya utajiri wake kufikisha tena zaidi ya dola trilioni moja za Marekani, kufuatia kupanda kwa thamani ya hisa za Kampuni zake za Tesla na SpaceX. Kwa mujibu wa Forbes, utajiri wa Musk ulifikia dola trilioni moja.
Jumatatu, Oktoba 5, 2026, baada ya kuongezeka kwa dola bilioni 30.6 ikilinganishwa na ljumaa iliyopita. Musk anaendelea kuwa Mtu tajiri zaidi duniani, akifuatiwa na Jeff Bezos mwenye utajiri wa dola bilioni 371.5, huku Larry Page akishika nafasi ya tatu akiwa na dola bilioni 284.3. Hisa za Tesla zilipanda kwa zaidi ya asilimia moja, huku thamani ya SpaceX ikiongezeka kwa zaidi ya asilimia tano, ongezeko lililomsaidia Musk kurejea kwenye hadhi ya Mtu

