Vatican City imetoa picha za kwanza za Papa Francis akiwa ndani ya jeneza Papa Francis ameonekana akiwa ndani ya jeneza la wazi
la mbao, amevaa mavazi mekundu ya kipapa, kofia ya askofu (miter), na rosari mikononi mwake huku Katibu wa Jimbo la Vatican, Kardinali Pietro Parolin akisali juu yake.
Picha hizo zilipigwa ndani ya kanisa dogo la binafsi katika Casa Santa Marta, makazi yake ndani ya Vatican, ambako aliífariki dunia siku ya Jumatatu akiwa na umri wa miaka 88.