Site icon Bongo Plus

Vita Vikiendelea Uchumi Wa Dunia Utayumba

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema katika kipindi hiki ambacho Dunia inashuhudia misuguano na machafuko katika maeneo mbalimbali ambayo yanapelekea kupanda kwa gharama za maisha ikiwemo bei za bidhaa na mafuta, Taifa la Tanzania lilimuhitaji Waziri William Lukuvi kutokana na uzoefu wake wa Kiungozi ili ushauri wake uweze kulivusha Taifa.

Akizungumza wakati wa kumuaga Lukuvi Jijini Dar es salaam leo March 28,2026, Rais Samia amesema “Lukuvi alikuwa Kiongozi aliyegusa mioyo ya Watu ambaye daima hakusita kusema ukweli na kuchukua maamuzi yenye tija na maslahi kwa Taifa, Ndugu zangu katika kipindi hiki ambacho Dunia imejaa mvurago na machafuko tulihitaji Viongozi wenye uzoefu wa muda mrefu na waliofanya kazi maeneo mbalimbali Serikalini na kwenye siasa ili tuendelee na mawazo na ushauri, tulimuhitaji Lukuvi sasa kuliko jana lakini Mungu alimpenda zaidi”

“Katika kipindi hiki dunia yetu imejaa msugano ambayo kwa vyovyote vile yatapandisha hali ya maisha kuwa ngumu sio kwa Tanzania tu bali kwa Dunia, tumeanza kushuhudia upandaji wa bei za mafuta na tutashuhudia upandaji wa bei za bidhaa na kama vita hii itendelea tunategemea kuwa na mdororo wa uchumi Duniani, mambo ambayo yanataka umakini katika kufanya maamuzi katika Uongozi wa Nchi yetu, tumuombe Mungu haya yamalizike ili twende vizuri”

“Kwa uzoefu alionao Lukuvi tulimuhitaji sasa kuliko wakati wowote, kwasababu tunamkumbuka kwa moyo wa upendo pamoja na utayari wa kushirikiana na Watu katika maeneo mbalimbali, huu ndio urithi aliotuachia Mpendwa wetu Mh. Lukuvi”

Exit mobile version