Site icon Bongo Plus

Waenda Kuokoa Ndege Iliyo Anguka Barabarani

Mtu mmoja amefariki dunia na wengine watano kujeruhiwa baada ya Ndege ya biashara aina ya Cessna Citation Latitude kuanguka kwenye barabara kuu ya Loop 20 Mjini Laredo, Jimbo la Texas Nchini Marekani usiku wa kuamkia Jumatano.

Ndege hiyo iliyokuwa ikiendeshwa na Kampuni ya NetJets, ilikuwa imebeba Watu sita na ilikuwa ikisafiri kutoka San Jose del Cabo Nchini Mexico kuelekea Austin, Texas, kwa mujibu wa taarifa za awali, Rubani aliripoti matatizo ya kiufundi akiwa angani na kuamua kuelekeza Ndege hiyo Laredo kwa ajili ya kutua kwa dharura.

Hata hivyo, Ndege hiyo ilianguka kwenye barabara kuu, ikigonga gari kabla ya kugonga kingo za usalama za barabara ambapo Mashuhuda walikimbilia eneo la tukio na kuwasaidia baadhi ya abiria kutoka ndani ya mabaki ya Ndege kabla moto haujaanza kuiteketeza.

Vikosi vya Uokoaji na Zimamoto vilifika haraka katika eneo la ajali, huku Mamlaka zikifunga barabara hiyo kwa shughuli za uokoaji na uchunguzi, Wataalamu kutoka Bodi ya Kitaifa ya Usalama wa Usafiri (NTSB) pamoja na Mamlaka ya Usafiri wa Anga ya Marekani (FAA) wameanza uchunguzi kubaini chanzo halisi cha ajali hiyo.

Exit mobile version