WAFAHAMU WAPINZANI WA YANGA KWENYE KUNDI “D” CAF CHAMPIONS LEAGUE.
AL AHLY.
Timu yenye mafanikio kuliko zote Afrika kwenye kila angle kuanzia nje hadi ndani ya uwanja,mabingwa mara 11 wa CAF champions league ikiwa ndio timu inayoongoza kwa kulitwaa taji hili huku pia wakiwa ni defending champion wa taji hili baada ya kulitwaa msimu uliopita.kizungumzia CAF champions league basi umeizungumzia Al Ahly,Cairo. Kwenye kundi “D” hawa ni favourite wanaweza kushindana na timu yoyote kwenye kundi lao na wakapata matokeo, ubora wao unajulikana hivyo Yanga inaenda kukutana na ladha halisi ya soka la Afrika kwani itacheza na bingwa wa CAF champions league mara 11.Kwenye hatua hizi Al Ahly wanakuwaga sio wagumu sana lakini sio kigezo cha kutowapa nafasi ya kufanya vizuri kwenye hili kundi bado wanabaki kuwa favourite.
CR BELOUIZDAD.
Mabingwa wa soka la Algeria ambao kwenye michuano ya Afrika sio haba wanathubutu kuonyesha ushindani mkubwa sana,misimu mitatu nyuma yote walifanikiwa kucheza hatua ya robo fainali ya CAF champions league. Hii inaonyesha jinsi gani wana uimara na muendelezo mzuri kwenye michuano hii kwa kipindi cha hivi karibuni. Hatua ya makundi kwao sio kitu kigeni tayari wameshazoea kucheza hatua hizi na hapo ndipo wanaizidi Yanga kete, kwani uzoefu pia ni kitu kinachoweza kuibeba timu kwenye mashindano haya.Ubora wao unaweza kuwapa challenge Yanga kufuzu kwenye hili kundi hivyo Yanga inatakiwa ku-pull up socks ili kuweza kushindana na CR Belouizdad ambao wanonekana ndio mpinzani mkubwa kwa Yanga kwenye kundi hili baada ya Al Ahly.
MEDEAMA SC.
Timu changa kwenye soka la Afrika,2008 ndio mwaka iliyoanzishwa inashiriki ligi kuu ya Ghana.imefuzu hatua hii ya group stage kwa kuitoa klabu ya Horoya ambayo msimu uliopita ilicheza hatua hii ya makundi,hivyo Medeama sio timu ya kubeza kwani imeitoa timu yenye uzoefu kwenye CAF champions league. Kwenye mashindano haya Medeama sio timu zoefu ndo kwanza inatafuta uzoefu,kucheza na Yanga ambayo tayari ilishafanya makubwa kwenye CAF confederation cup msimu uliopita basi kuna faida ya uzoefu Yanga wanayo dhidi ya kuikabili Medeama.Kwenye kundi hii ndio timu ambayo haijaizidi chochote Yanga kw