Site icon Bongo Plus

Wafanyakazi Wanatakiwa kufuta Viwakilishi vya Jinsia

Serikali ya Marekani imeagiza wafanyakazi wa mashirika mbalimbali ya serikali kuondoa
viwakilishi vya kijinsia (pronouns) kutoka kwenye sahihi zao za baruapepe ifikapo ljumaa Januari 31.

Agizo hilo limetolewa kupitia nyaraka za ndani zilizopatwa na ABCNews, likihusishwa na maagizo mawili ya kiutendaji
yaliyosainiwa na Rais Donald Trump siku yake ya kwanza madarakani, yakilenga kupunguza programu za utofauti
(diversity) na usawa (equity) serikalini.


Katika ujumbe uliotumwa kwa wafanyakazi wa Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa (CDC) jumaa asubuhi, wafanyakazi waliamriwa kuondoa viwakilishi vya kijinsia
na taarifa zingine ambazo haziruhusiwi kwa mujibu wa sera mpya.

Agizo ama hilo pia lilitolewa kwawafanyakazi
wa ldara ya Usafirishaji (DOT) na Idara ya Nishati (DOE), likihusiana na agizo la Trump la kuondoa lugha ya DEI (Diversity, Equity, and Inclusion) katika mawasiliano rasmi
ya serikali.

Hadi sasa, haijafahamika iwapo mashirika mengine ya serikali pia yamepokea maagizo kama haya. Hatua hii linatajwa kuwa sehemu ya jitihada za utawala wa Trump kufuta juhudi za DEl serikalini na kurejesha kile
wanachokita “ukweli wa kibaolojia.”

Exit mobile version