Site icon Bongo Plus

Waliokuwa Nje Nikawaambia Warudi, Saivi Wananitukana.

“Ni hawa waliomba kuja kuniona nikawapokea. Tukazungumza walikuwa hawana hata shilingi. Nilitoa kiposho changu nilichogaiwa cha safari niliwapa waendelee na maisha wakiwa nje. Ni hawa hawa waliniambia watarudi nchini lakini wana kesi.

“Niliwaambia kwamba kesi nitazifuta. Njooni tukae tuizungumze tujenge nchi. Kulikuwa na baadhi yao walikuja mikoni mitupu. Hawana kitu. Tulitoa fedha zetu kuwapa waanzie maisha hapa Tanzania.

“Nataka mumpe cheo mtu wa namna hiyo aliyenyooshewa mkono wote huu wa rehema na upatanishi. Yule alimnyooshea ndio wa kwanza kumkashifu. Kumtukana kugeuza mambo na kuichafua nchi. Niliwapa fursa zote. Ninyi mashahidi. Niliwapa fursa ya kufanya shughuli zao za kisiasa”- Rais Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wazee wa mkoa wa Dar es Salaam.

Exit mobile version