Site icon Bongo Plus

Wanaume 95% Wanataka Amani Kuliko Uzuri wa Mwanamke.

Ripoti mpya kutoka Global Wellness Institute imebainisha kuwa asilimia 95 ya wanaume mwaka 2025 kuwa katika mahusiano yanayowaletea amani ya akili badala ya kuvutiwa na urembo wa nje pekee.

Hii inaonyesha mabadiliko makubwa ya mitazamo, ambapo wanaume wengi sasa wanathamini utulivu wa kihisia, mawasiliano yenye maana, na mazingira salama ya kiakili katika mahusiano ya kimapenzi.

Katika enzi hii ya uponyaji wa kihisia, wanaume wengi wanasema wamechoka na mahusiano yenye migogoro isiyoisha, na sasa wanatafuta washirika wanaochangia utulivu na maendeleo ya pamoja.

Hali ya mahusiano yako ipoje 2025. Uzuri kwanza au Amani ndio unaipa kipaumbele?

Exit mobile version