Jeshi la Polisi Mkoani Iringa Limesema limewakamata Watuhumiwa watatu kufuatia mauaji ya aliyekuwa Katibu wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Kilolo Mkoani Iringa aliyeuawa kwa kupigwa Risasi.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Kamanda wa Polisi Mkoani Iringa Allan Bukumbi amesema tayari Watuhumiwa watatu wamesha kamatwa na upelelezi ukikamilika watafikishwa Mahakamani kwaajili ya hatua zaidi za kisheria.
Kiukweli tukio la Katibu wa CCM linaendelea Vizuri na tumeshawakamata Watuhumiwa kadhaa na wengine baada ya kubaini kuwa hawahusiki basi tuliwaachia ila upelelezi Bado unaendelea na hatua za mwisho zikikamilika basi tutawataarifu ” Amesema Allan Bukumbi
Ikumbukwe tarehe 13 November Katibu wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Kilolo Christina Kibiki aliuawa kwa kupigwa Risasi na Watu ambao hawakufahamika nyumbani kwake.