bWaziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Paul Makonda, amekabidhi Bendera ya Taifa kwa timu ya mpira wa kikapu ya Dar City ikiwa ni ishara ya uwakilishi wa nchi kwa timu hiyo inayokwenda kushiriki mashindano makubwa ya Basketball Africa League (BAL) nchini Afrika Kusini.
Akizungumza wakati wa hafla ya kuaga timu hiyo, leo Machi 23, Jijini Dar es Salaam Waziri Makonda alieleza kuwa, Serikali ina imani kubwa na uwezo wa wachezaji hao kufanya vizuri na kuipeperusha vyema bendera ya Tanzania katika mashindano hayo.
Amewataka wachezaji kuzingatia nidhamu, mshikamano na uzalendo ili kufikia malengo waliyojiwekea.
Aidha, wachezaji wa Dar City wameahidi kupambana kwa juhudi zote kuhakikisha wanaleta matokeo bora na kuiwakilisha vyema Tanzania kupitia mashindano hayo.
