Waziri wa Afya Mhe. Mohamed Mchengerwa ambaye ni mgeni rasmi akiwasili kwenye kongamano kuu la mwaka la kisayansi la 33 linalofanyika hapa Jijini Arusha.
Waziri Mchengerwa amemuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kongamano hilo ambalo limelenga kuleta faida kubwa kwa nchi kwenye masuala ya tafiti na kada ya sayansi kwa ujumla linalofanyika kati ya tarehe 9 hadi 11 Juni, 2026.
