Site icon Bongo Plus

Waziri wa Afya Mheshimiwa Jenista Mhagama leo Machi 24, 2025 amewasili katika Ofisi za Ubalozi wa Tanzania katika Jamhuri ya Zambia zilizopo Jijini Lusaka

Waziri wa Afya Mheshimiwa Jenista Mhagama ambaye pia ni Mjumbe Maalum wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt Samia Suluhu Hassan leo Machi 24, 2025 amewasili katika Ofisi za Ubalozi wa Tanzania katika Jamhuri ya Zambia zilizopo Jijini Lusaka na kupokelewa na Mheshimiwa Balozi Luteni Generali Mathew Edward Mkingule.

Waziri Mhagama anatarajia kuwasilisha ujumbe maalum wa Rais Samia kwa Rais wa Jamhuri ya Zambia Mheshimiwa Haikainde Hichilema hapo baadae siku ya leo.

Exit mobile version