Masaa machache yamepita tangu Msanii @gnakowarawara kuvujisha ngoma mpya ya kundi la Weusi, kitendo hicho kimemuibuka Rapa wa kundi hilo Joh Makini ambae ameonyesha kutopendezwa kabisa kupitia ukurasa wake wa X (Twitter) ameandika 👇🏻
“Hatuwezi kutoa miziki kiholela kwa kujaribu kama Pipii hizi sio piano bana” @johmakinitz
Majibizano hayo yameonyesha kuwa hakuna maelewano mazuri kwenye suala la kuachia wimbo wa kundi lao la Weusi.
Kama mbwai mbwai tu, @gnakowarawara ameishinda vita rasmi ameidondosha ngoma mpya ya Weusi inayoitwa “Hii Hapa” nenda ka-enjoy nayo. Japo kwa @johmakinitz @lordeyesmweusi hawakuridhika kabisa na wimbo huo kutoka.