Ikulu Ya Marekani Yamkosoa Serena Kulilia Wahamiaji
Ikulu Ya Marekani Yamkosoa Serena Kulilia Wahamiaji.
Msanii wa Kimarekani mwenye asili ya Mexico, Selena Gomez, amejikuta katika utata baada ya kuchapisha video kwenye Instagram akilia kwa huzuni kuhusu kuondolewa kwa wahamiaji wasiokuvwa na vibali nchini Marekani.
Baada ya video hiyo kusambaa, utawala wa Trump ulitoa video yenye kichwa “Mama wa Wahanga wa Wahamiaji Haramu Wamshambulia Selena Gomez: Hukulia kwa Ajili ya Mabinti Zetu” ikimkosoa vikali SelenaGomez huku ikionyesha akina mama wa watu waliouawa na wahamiaji wasio halali wakimshutumu kwa upendeleo.
Selena Gomez alifuta video yake ya mwanzo lakini alijibu kwa kusema, “Inaonekana si sawa kuonyesha huruma kwa watu.”
Rais wa Marekani, Donald Trump amekuwa akitekeleza sera kali za uhamiaji, ikiwa ni pamoja na kusaini Laken Riley Act, ambayo inalenga kuwapa adhabu kali wahamiaji wasiokuwa na vibali wanaofanya uhalifu.
Pamoja na lawama anazopokea, Selena Gomez ameendelea kuunga mkono haki za wahamiaji, akisema, “Ninataka kusimama na watu wangu.