MFAHAMU MNYAMA #FISI ALIVYO, SEHEMU YA KWANZA (FACTS ABOUT HYENA PART1)

 

SEHEMU YA 1.

UTANGULIZI.
Fisi ni jamii ya wanyama wala nyama, wengi tunamfahamu kama bwana afya wa porini. Hujulikana kwa kula mizoga japo hawa ni wawindaji wazuri sanaaa. Hula mizoga pale wakizidiwa.

Hii ya kula mizoga inasababishwa na mengi, nitakueleza kadri tunavyoendelea na makala hii kwa undani. Tuanze sasa taratibu.

INASEMEKANA NI WAZAZI WAZURI SANA.
Wataalamu wa wanyama wanamwelezea fisi kuwa ni miongoni mwa wanyama wenye akili, na mzuri zaidi kwenye malezi ya watoto wao. Ni wanyama ambao wapo makini sana na watoto.

Fisi anapokuwa na watoto huwa hachezi mbali na wanae. Muda wote anahakikisha watoto wapo salama. Watoto huwa wanalindwa kuliko maelezo kwa kufichwa kwenye mapango ama mashimo.

CHAKULA CHA WATOTO HUWA HAKIGUSWI.
Hata kama wao watakosa chakula ni bora wafe wote. Ila watoto watahifadhiwa chakula chao na hakiguswi na fisi yeyote yule. Ukigusa chakula cha watoto ni kipigo, au upewe adhabu na ikiwezekana unafukuzwa kwenye kundi ukaishi kwingine.

KIONGOZI KWENYE KUNDI HUWA NI JIKE.
Kwa fisi, kundi huongozwa na jike mkubwa. Yeye ndo hupanga na kuratibu mambo tofauti kwenye kundi ikiwemo kugawa majukumu ya kila siku. Inapotokea mmoja wao kashindwa kufuata taratibu basi hupewa adhabu. Moja ya adhabu ni kung’atwa sikio. Ikiwa adhabu inatakiwa iwe kali zaidi, basi hufukuzwa kwenye kundi. 😁✋

ANA MAZIWA YENYE PROTINI NYINGI.
Wataalamu wa wanyama wanasema anaongoza kwa kuwa na maziwa yenye protini nyingi kuliko wanyama wote wala nyama mbugani. Sijabahatika kuyapata maziwa yake nikayaonja, ila kama nitabahatika kuyapata, nitaleta taarifa zaidi kuhusu hili. Tuendelee kuwa wavumilivu.

MAUMBILE YA UZAZI YA FISI JIKE.
Hapa naomba niongezee tu kusema “Maumbile ya uzazi ya fisi jike yanafanana (hayako sawa) na yale ya fisi dume. Wanaita pseudo penis. Muonekano ni sawa ila kazi ni tofauti na ile ya fisi dume.

 

Makala hii imedhaminiwa na winn licious

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button