Marioo Atoa Baraka Zake kwa Chino Wana Man, Amuombea Dua Awemkubwa

Marioo Atoa Baraka Zake kwa Chino Wana Man,Amuombea Dua Awemkubwa.

Msanii wa Bongo Fleva, Marioo_tz, ameonyesha upendo kwa kuwatakia heri ya kuzaliwa Chino Kidd, lamstans_tz, na Abdwambelele kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Marioo, ambaye alikuwa akihusishwa kuwa na bifu na Chino Kidd, aliandika:

“Mungu Awabariki Mfanikiwe zaidi. Chino Ulipotoka na Mpaka kufikia mafanikio uliyonayo we ni Mfano mzuri kwa vijana wenye ndoto na wapambanaji Keep it up

Kwa Stans, Marioo alimpongeza kwa kipaji chake kikubwa na nidhamu ya hali ya juu, huku akimwambia Abdwambelele kwamba anathamini utendaji na nidhamu yake kazini.

Ujumbe huu unaonyesha ukomavu wa Marioo na upendo wake kwa watu wake wa karibu, hata kwa Chino Kidd, licha ya tofauti zilizotokea mwaka jana.

Hii ni ishara ya mshikamano na heshima ndani ya kiwanda cha muziki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button