Harmonize Akiri Hakuna Yeye Bila Rais Samia

Harmonize Akiri Hakuna Yeye Bila Rais Samia

Harmonize ameonyesha mapenzi heshima zake kwa Rais Samia Suluhu Hassan kupitia ujumbe mzito wa shukrani na furaha katika siku ya kuzaliwa kwa Rais huyo mpendwa. Kupitia ukurasa wake wa Instagram,

Harmonize aliandika, “Kama humpendi, achana na mimi! Bila huyu mama No @samia_suluhu_hassan No KONDE O HAPPY BIRTHDAY MY PRESIDENT.

Nakutakia kampeni njema!! Tunataraji ushindi wakishindo na si mwingine ni Samia tena!!!” Harmonize pia aliahidi kushea zaidi nyakati za kipekee za maadhimisho hayo, huku akiwasihi mashabiki wake kubaki wakifuatilia ukurasa wake kwa taarifa zaidi.

Kwenye ujumbe huo, Harmonize alisisitiza mchango mkubwa wa Rais Samia si tu kwa maendeleo ya taifa, bali pia kwa wasani na sekta ya burudani. Kwa hakika, Harmonize amekiri upendo na uungaji mkono wake kwa rais na uongozi wake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button