Nyimbo 10 Bora za Apple Music Tanzania

Nyimbo 10 Bora za Apple Music Tanzania

Nyimbo 10 bora za Apple Music Tanzania
zinazoendelea kuvutia mashabiki wa muziki wanaoishi Tanzania ni kama ifuatavyo:

1. Kwenye nafasi ya kwanza ni kolabo kali ya @juma_jux @DiamondPlatnumz, Ololufe Mi. Huu ni wimbo mwingine wenye mafanikio kutoka kwa wasani hawa wawili ambao mwaka jana waliumiliki mwaka na Enjoy.

2. @marioo_tz na msanii wake wa @badnationtz, @iamstans_tz, wamepoteza nafasi ya juu kwa Ololufe Mi, lakini wimbo wao 2025 bado unashikilia nafasi ya pili.

3. @officialnandy na mume wake @billnass wanaendelea kuvutia hisia za wapendanao na mashabiki wao kupitia wimbo wao Totorimi.

4. Zuchu, Dada mkuu wa (@wcb_wasafi anaendelea vizuri na wimbo wake mpya Pwita, ambao unakimbia kimyakimya lakini kwa kasi.

5. Extra Pressure wa @Bensoulmusic na @bienaimesol umepanda kutoka nafasi ya Saba hadi nafasi ya tano, ukipambana kurudi kwenye kilele cha chati baada ya kuongoza wiki zilizopita.

6. @darassacmg255 na Harmonize wanashika nafasi ya sita na wimbo wao Mazoea, wakionyesha ukuaji wa haraka kulinganisha na uchanga wa wimbo wao.

7. Harmnonize ameendelea kuwepo na wimbo wake You Better Go, ambao unashikilia nafasi ya saba, akionekana
kuweka mkazo kwenye mchuano wa kumi bora hii.

8. Ogechi (Remix) kutoka kwa BoyPee, Hyce, na Brown Joel wakimshirikisha Davido inashika nafasi ya nane, wakiwa wanatisha kwenye chati na remix yao.

9. Chris Brown bado yupo ndani ya Top 10 na wimbo wake Angel Numbers / Ten Toes. Ameendelea kubadili nafasi tu, lakini tangu Novemba 2023 hajawahi kuondoka
kwenye chati hii.

10. Nafasi ya kumi inashikiliwa na Nani @itsdvoice akimshirikisha Zuchu. Wimbo huu unafunga orodha ya nyimbo 10 bora kati ya nyimbo 100 bora za Apple Music
Tanzania.

Hata hivyo @harmonize_tz na @officialzuchu ndio wasanii pekee waliojitokeza mara mbili kwenye chati hii, kila mmoja akiwa na wimbo wake binafsi na wimbo wa kushirikishwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button