Diddy Anyimwa Dhamana Alitoa Ofa ya Tsh BIL 136+
Diddy Anyimwa Dhamana Alitoa Ofa ya Tsh BIL 136+


Diddy will remain behind bars as he faces federal charges.
_______________________________________
Rapa Na Mfanyabiashara ‘Diddy’ Ameripotiwa Kunyimwa Dhamana Baada Ya Kudai Kuwa Hana Hatia Katika Mashtaka Ya Kingono Yanayomkabili Na Hivyo Ataendelea Kubaki Rumande Hadi Pale Kesi Yake Itakapoanza Kusikilizwa.
Imeelezwa Kuwa Diddy Alitoa Ofa Ya Dola Mil 50 (Tsh Bil 136+) Na Kuisalimisha Passport Yake lli Atolewe Kwa dhamana Lakini Ombi Hilo Lilipigwa Chini Jaji Wa Mahakama Ya Manhattan ‘Robyn F. Tarnofsky’.
Kwenye Ofa Ya Dhamana Hiyo Diddy Aliweka Nyumba Yake Ya Miami Yenye Thamani Ya Dola Mil 48 Pamoja Na Mjengo Wa Mama Yake Wenye Thamani Ya Dola Mil 2 ili Kukamilisha Kiasi Alichotaja Kukitoa.
Pia Waendesha Mashtaka Waligoma Kuachiwa Kwa Diddy Wakidai Kuwa Ni Hatari Kwa Jamii.
Kumbuka Jana Rapa Huyu Aliripotiwa Kukamatwa Na Maafisa Usalama Wa New York Kama Sehemu Ya Uchunguzi Wa Kesi Zilizofunguliwa Dhii Yake Kama Vile Kuwatumikisha Mabinti Wadogo Kingono, Udhalilishaji N.k





