Watoto wa P Diddy King Combs na Justin Mahakamani Kumtembelea Baba Yao

Watoto wa P Diddy King Combs na Justin Mahakamani Kumtembelea Baba Yao

Baada ya Baba yao kukamatwa siku ya jana, King Combs pamoja na kaka yake Justin Dior Combs walionekana kuingia Mahakamani huko New York kwa lengo la kumtembea baba yao akiwa chini ya Ulinzi.

Ikumbukwe kuwa Diddy alikamatwa katika eneo la Manhattan New York baada ya kuzingirwa kwa makazi yake ya Los Angeles na Miami ikiwa ni sehemu ya uchunguzi unaoendelea, mitandao ya AFP The New York Times, CNN ,TMZ na mingine Nchini Marekani iliripoti.

Diddy amekamatwa ikiwa imepita miezi kadhaa tangu EX wake ambaye ni Mwimbaji Cassandra Ventura (Cassie) alipofungua kesi akimtuhumu Diddy kwa ubakaji na unyanyasaji wa Kingono kipindi chote cha mahusiano yao yaliyoanza miaka 20 iliyopita.

Baadaye Jumba la kifahari la Diddy likazingirwa mwezi March mwaka huu na Maafisa wa usalama ambao ilidaiwa walipanga kumkamata Diddy lakini hata hivyo hawakufanya hivyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button