MAKAMU WA RAIS AFANYA ZIARA NEMC
ASISITIZA WELEDI , BIDII YA KAZI, USHIRIKIANO NA UADILIFU
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi amewasihi watumishi wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), kufanya kazi kwa bidii, weledi, ushirikiano na kujiepusha na vitendo vya rushwa ili kuifanya Taasisi hiyo kuwa chachu ya uhifadhi wa mazingira na maendeleo ya Taifa.
Makamu wa Rais ametoa wito huo, alipofanya ziara Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Makao Makuu, Mikocheni Jijini Dar es Salaam. Amewataka watumishi kufanya kazi kwa uadilifu na kutokuwa kikwazo katika utekelezaji wa miradi mikubwa kwa kutanguliza maslahi ya Taifa mbele.
Makamu wa Rais ameipongeza NEMC kwa kutimiza miaka 40 tangu kuanzishwa kwake na kuendelea kuwa chombo kinachohitajika na kutumainiwa nchini.
Aidha, Makamu wa Rais ameipongeza NEMC kwa Mpango Mkakati wa miaka Mitano ambao umeanisha vitu mbalimbali vitakavyowezesha usimamizi na utunzaji wa mazingira kwa ufanisi. Amesema uanzishwaji wa mashindano ya uhifadhi wa mazingira ni muhimu kwa kuwa itakua hamasa ya upandaji miti na usafi kitaifa.
Vilevile, Makamu wa Rais amesema ili kudhibiti masuala ya uchafu ni vema pia kuwatambua wanaokuwa wamefanya vibaya katika mashindano ya usafi na kuwataja hadharani ikiwemo kupatiwa vyeti. Ameiagiza Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, kushirikiana na NEMC katika kufanikisha mashindano ya usafi na utunzaji mazingira nchini.
Halikadhalika Makamu wa Rais, ameitaka NEMC kutilia mkazo suala la nishati safi, matumizi ya teknolojia za kisasa katika kulinda mazingira pamoja na kusimamia vema suala la urejerezaji taka.
Makamu wa Rais, amewapongeza Viongozi wa NEMC kwa kuendelea na mchakato wa kuifanya NEMC kuwa Mamlaka kamili. Amesema suala hilo linashughulikiwa na katika kipindi cha Serikali ya Awamu ya Sita limepewa umuhimu wa kipekee.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Dkt. Emmaculate Sware amesema NEMC imeaandaa Mpango Mkakati wa miaka mitano yaani mwaka 2026/2027 – 2030/2031 ambao umelenga kuongeza ufanisi wa usimamizi wa mazingira, kuim






