Makonda: Tumeandaa mwongozo wa kuwarejesha kazini waandishi wakongwe walioathiriwa na JAB

Makonda: Tumeandaa mwongozo wa kuwarejesha kazini waandishi wakongwe walioathiriwa na JAB

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda amesema wizara kupitia Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari imeandaa mwongozo maalumu wa kisheria utakaowezesha wanahabari wakongwe walioathiriwa na mfumo wa ithibati kurejea katika mfumo rasmi.

“Mwongozo huu unaweka utaratibu wa kisheria wa kutambua na kuthibitisha umahiri wao kupitia tathmini maalumu ya uzoefu, weledi na maadili ya taaluma na kuwawezesha kupata ithibati kwa mujibu wa sheria,” amesema Makonda.

Makonda amesema hayo leo Jumatatu, Mei 4, 2026 bungeni jijini Dodoma wakati akiwasilisha bungeni makadirio ya mapato na matumizi ya wizara kwa mwaka wa fedha 2026/27.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button