Makonda aomba Sh525.32 bilioni kutekeleza vipaumbele tisa

Makonda aomba Sh525.32 bilioni kutekeleza vipaumbele tisa

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda ameomba Sh525.32 bilioni kwa ajili ya bajeti ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2026/27 kwa ajili ya kutekeleza vipaumbele tisa.

Miongoni mwa vipaumbele hivyo ni kukamilisha ukarabati, uboreshaji na ujenzi wa miundombinu, kukamilisha maandalizi ya AFCON 2027, pamoja na maandalizi ya kuwa mwenyeji wa Mashindano ya 74 ya Urembo ya Dunia (Miss World).

Vingine ni kukamilisha utungaji na uhuishaji wa sera, sheria, mikakati, miongozo na kanuni mbalimbali ili kuimarisha usimamizi na utekelezaji wa majukumu katika sekta hizo.

Mbali na kukuza na kustawisha Kiswahili kikanda na kimataifa, pia kuimarisha ushiriki wa timu za Taifa katika mashindano ya kimataifa, kuboresha elimu na mafunzo katika tasnia za utamaduni, sanaa na michezo, pamoja na kuratibu na kusimamia matamasha, shughuli na matukio makubwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button