Mfalme wa miaka 64 Afariki Upasuaji wa Kupunguza Unene Wafeli

Mfalme wa miaka 64 Afariki Upasuaji wa Kupunguza Unene Wafeli

Mfalme wa jadi wa jamii ya ljaw huko Nigeria, HRH Moses Theophilus, ametangazwa kufariki dunia jana akiwa na umri wa miaka 64. Taarifa zinaeleza kuwa kifo chake kilitokana na matatizo yaliyojitokeza baada ya upasuaji wa liposuction (upasuaji wa kuondoa mafuta mvwilini) ulioshindikana katika jimbo la Bayelsa, nchini Nigeria.

Kulingana na vyanzo vya habari, mfalme huyo alikuwa akifanyiwa upasuaji huo, lakini hali yake ilizorota na kusababisha kifo chake. Jamii ya ljaw na familia yake imepatwa na msiba huo mzito. Taarifa zaidi kuhusu mazishi na maisha yake zinatarajiwa kutolewa na viongozi wa jadi wa eneo hilo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button