Kweka Apanda Kizimbani Tuhuma za Kumuuwa Mkewe na Bastola

Kweka Apanda Kizimbani Tuhuma za Kumuuwa Mkewe na Bastola

Mfanyabiashara na mkazi wa Bunju A, jijini Dar es Salaam, Laurence Kweka (48), amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni akikabiliwa na shtaka la kumuua mkewe, Jane Maloo Urassa, kwa kumpiga risasi.

Kweka amesomewa shtaka hilo leo Alhamisi, Oktoba 15, 2026, na Wakili wa Serikali, Harrison Lukosi, mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Kemilembe Josiah. Wakili Lukosi amesomea shtaka hilo katika kesi ya mauaji namba 23407 ya mwaka 2026. Kabla ya kusomewa shtaka hilo, Hakimu Josiah alimweleza mshtakiwa kuwa hatakiwi kujibu chochote mahakamani hapo kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi za mauaji.

Pia, hakimu alimweleza kuwa shtaka la mauaji analokabiliwa nalo halina dhamana kwa mujibu wa sheria, hivyo ataendelea kusalia rumande hadi upelelezi utakapokamilika. Akisoma shtaka hilo, Lukosi alidai Kweka anatuhumiwa kutenda kosa hilo kinyume na vifungu vya 196 na 197 vya Sheria ya Kanuni ya Adhabu, Sura ya 16, iliyofanyiwa marejeo mwaka 2023. Alidai mshtakiwa huyo alitenda kosa hilo Oktoba 1, 2026, katika eneo la Bunju A, Wilaya ya Kinondoni, Mkoa wa Dar es Salaam, ambapo anadaiwa kumuua Jane Maloo Urassa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button