Sio Rahisi kuishambulia Iran Kwasasa Asema Netanyau

Sio Rahisi kuishambulia Iran Kwasasa Asema Netanyau

Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu amesema kwamba shambulio jipya la Marekani au lsraeli dhidi ya Iran halitakuwa rahisi kwa lsraeli kwa sasa, siku chache kabla ya uchaguzi wa nchi hiyo wa Oktoba 27. “Kwa maoni yangu, hilo si jambo rahisi kwetu,” Netanyahu aliambia Redio ya jeshi alipoulizwa kuhusu uwezekano wa shambulio dhidi ya Iran katika siku zijazo.

Hakufafanua zaidi. Maoni yake yalikuja siku moja baada ya Channel 12 ya lsraeli kuripoti kwamba Netanyahu alikuwa amemshinikiza Rais wa Marekani Donald Trump kufufua mapigano na Iran kabla ya uchaguzi wa Israeli na muhula wa kati wa Marekani. Ofisi ya Netanyahu ilikanusha kwamba alikuwa akitaka kuanzisha vita kabla ya kura.

Ikumbukwe kuwa Trump alisema Jumanne kwamba utawala wake utafanya uamuzi kuhusu Iran “hivi karibuni.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button