Mfungwa Aliyenusurika Sindano ya Kifo aanza kutembea
Mfungwa Aliyenusurika Sindano ya Kifo aanza kutembea
Christa Pike (50), mwanamke aliyenusurika jaribio la kunyongwa kwa sindano ya sumu nchini Marekani, ameanza kutembea ndani ya chumba chake hospitalini, huku akiendelea kupata athari za dawa aliyopewa wakati wa utekelezaji wa hukumu hiyo ulioshindikana.
Pike alinusurika baada ya sindano mbili za dawa ya sumu kutolewa Septemba 30, mwaka huu katika Jimbo la Tennessee, tukio ambalo limeelezwa kuwa la nadra katika historia ya utekelezaji wa hukumu za kifo. Wakili wake, Stephen Ferrell, aliambia BBC kuwa Pike bado ana hali ya kuchanganyikiwa kiakili, lakini ameanza kutembea mwenyewe ndani ya hospitali. “Ameanza kutembea kwa mara ya kwanza leo, lakini ni ndani ya chumba tu na si umbali mrefu,” amesema Ferrell, akisema taarifa hizo amezipata kutoka kwa watu waliomtembelea Pike.
Ferrell amesema hali ya Pike imeanza kuimarika ikilinganishwa na siku za awali, baada ya kulazwa akiwa katika hali mbaya na kupoteza fahamu. Hata hivyo, amesema Pike bado ana majeraha makubwa mikononi yanayomfanya ashindwe kuyatumia vizuri, huku akiendelea kupata athari za dawa ya pentobarbital iliyodungwa mwilini wakati wa utekelezaji wa hukumu.





