NCMC.YAVUTIA UWEKEZAJI BIASHARA YA KABONI COP31

  1. Antalya, Uturuki – 11 Novemba 2026
    Kampuni ya Carbon Bridge imekutana na wataalamu wa Kituo cha Taifa cha Ufuatiliaji wa Kaboni (National Carbon Monitoring Centre – NCMC) katika mkutano wa pembezoni mwa Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi (COP31) unaoendelea jijini Antalya, Uturuki, kwa lengo la kujadili fursa za uwekezaji na kuimarisha ushirikiano katika kuendeleza miradi ya kimkakati ya biashara ya kaboni nchini Tanzania.
    Katika majadiliano hayo, Carbon Bridge imeeleza kuvutiwa na fursa zilizopo nchini Tanzania katika sekta ya biashara ya kaboni ambapo itawekeza katika miradi ya kimkakati ya Biashara ya kaboni, ikitambua mazingira rafiki ya uwekezaji, uwepo wa fursa nyingi za miradi inayoweza kuzalisha viwango vikubwa vya kabni (Carbon credits), pamoja na mfumo wa uratibu na usimamizi wa biashara ya kaboni unaosimamiwa na Serikali kupitia NCMC.
    Kwa upande wake, wataalamu wa NCMC wameihakikishia kampuni hiyo ushirikiano wa kitaalamu na uratibu katika hatua mbalimbali za uwekezaji na utekelezaji wa miradi ya biashara ya kaboni, kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na miongozo ya Serikali inayosimamia sekta hiyo nchini.Aidha; wamefafanua kuwa tayari kampuni hiyo imeshafanya uwekezaji kwenye biashara ya kaboni katika sekta ya Nishati safi ya kupikia pamoja na katika majiko yaliyoboreshwa.
    Aidha, majadiliano hayo yamelenga kubainisha maeneo ya kimkakati ya uwekezaji, kuimarisha uratibu kati ya Serikali na wawekezaji, pamoja na kuhakikisha miradi inayotekelezwa inazingatia viwango vya uadilifu wa kaboni inaleta manufaa ya kiuchumi na kijamii kwa wananchi na kuchangia juhudi za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.
    Kwa sasa, Tanzania inaendelea kufungua fursa za uwekezaji katika biashara ya kaboni kupitia sekta mbalimbali zikiwemo misitu, kilimo, nishati, maji na usimamizi wa taka. Sekta hizo zina uwezo mkubwa wa kuvutia uwekezaji, kuzalisha viwango vya kabaoni, kuongeza kipato, kwa jamii na kuchochea maendeleo endelevu nchini.
    NCMC ni taasisi iliyo chini ya Ofisi ya Makamu wa Rais, iliyoanzishwa kwa lengo la kuratibu, kusimamia na kufuatilia utekelezaji wa biashara ya kaboni nchini Tanzania. Taasisi hiyo pia ina jukumu la kutoa ushauri wa kitaalamu, kufuatilia usajili na utekelezaji wa miradi pamoja na kuhakikisha taarifa za miradi ya biashara ya kaboni zinazingatia mifumo na taratibu zilizowekwa na Serikali.
    Ushiriki wa NCMC katika majadiliano hayo ni sehemu ya juhudi za Serikali za kuitangaza Tanzania kama kituo kinachovutia uwekezaji wa biashara ya kaboni, kuimarisha ushirikiano na wawekezaji wa kimataifa na kuhakikisha rasilimali za nchi zinatumika kwa tija kupitia uwekezaji wenye uadilifu na manufaa kwa taifa.
    Washiriki wa Mkutano huo kutoka NCMCni; Mkurugenzi wa Idara ya Ufuatiliaji, Usajili na Utoaji Taarifa za Miradi, Dkt. Deo Shirima; Mkurugenzi wa Idara ya Usalama wa Mazingira, Ushauri na Utafiti Dkt. Paul Lyimo, Mkurugenzi wa Kitengo cha Sheria, Bi. Risper Koyi; pamoja na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano, Ibrahim Hamidu.
    Kwa upande wa Kampuni ya Carbon Bridge, washiriki walikuwa Marion Verles, Afisa Mtendaji Mkuu ; Donee Alexander, Afisa Mkuu wa Masuala ya Kaboni na Fabio Marque, Mkurugenzi wa Sera na Maendeleo ya Biashara
{“source_type”:”vicut”,”data”:{“client_key”:”aw889s25wozf8s7e”,”source_type”:”vicut”,”source_platform”:”mobile_2″,”appVersion”:”19.9.0″,”enterFrom”:”new_image”,”os”:”android”,”product”:”vicut”,”editType”:”image_edit”,”region”:”GB”,”picture_id”:”MP0Q229V-Q6W2-ET77-BSP4-NRJI9ORL5X6E”,”pictureId”:”MP0Q229V-Q6W2-ET77-BSP4-NRJI9ORL5X6E”,”capability_name”:”capcut_photo_editor”},”tiktok_developers_3p_anchor_params”:”{“client_key”:”aw889s25wozf8s7e”,”source_type”:”vicut”,”source_platform”:”mobile_2″,”appVersion”:”19.9.0″,”enterFrom”:”new_image”,”os”:”android”,”product”:”vicut”,”editType”:”image_edit”,”region”:”GB”,”picture_id”:”MP0Q229V-Q6W2-ET77-BSP4-NRJI9ORL5X6E”,”pictureId”:”MP0Q229V-Q6W2-ET77-BSP4-NRJI9ORL5X6E”,”capability_name”:”capcut_photo_editor”}”}

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button