RAISMZEE KUGIA AKABIDHIWA BAJAJI
“NAMSHUKURU RAIS SAMIA” — MZEE KUGIA AKABIDHIWA BAJAJI
“Nilikuwa na mawazo, nilikuwa silali… Sasa Mungu ameniona kupitia kwako, kupitia Samia namshukuru.”
Hizi ni shukrani za Jonas Machilu Seni Kugia, aliyepata ulemavu baada ya kugongwa na bajaji, baada ya Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba, kumkabidhi bajaji ya kumsaidia kujipatia kipato.
Mzee huyo ametoka Musoma hadi Kahama kuwasilisha ombi lake, ambalo limetekelezwa siku hiyo hiyo baada ya Waziri Mkuu kumsikiliza katika mkutano wa hadhara.
🗓️ Novemba 10, 2026
📍 Kahama, Shinyanga





