Jiji la Arusha Lachunguza Kifo cha Mgonjwa Kaloleni
Jiji la Arusha Lachunguza Kifo cha Mgonjwa Kaloleni
Halmashauri ya Jiji la Arusha imeunda timu maalumu ya kuchunguza tuhuma za uzembe wa wahudumu wa afya katika Hospitali ya Kaloleni, zinazohusishwa na kifo cha Esther Mrema, mkazi wa Njiro jijini humo. Mrema alifariki dunia Oktoba 27, 2026, baada ya kulazwa katika hospitali hiyo tangu Oktoba 20, mwaka huu, akisumbuliwa na nimonia kali.
Familia ya marehemu inadai kuwa kuchelewa kubadilishwa kwa mtungi wa oksijeni hali ya mgonjwa ilipozidi kuwa mbaya kulichangia kifo chake. Kutokana na tuhuma hizo, Mkurugenzi wa Jiji la Arusha, John Kayombo ameunda timu ya kuchunguza mazingira ya tukio hilo.
Katika taarifa iliyotolewa jana Oktoba 28, 2026, Halmashauri ya Jiji la Arusha ilieleza imeanza kuchunguza tukio hilo kufuatia taarifa zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu kifo cha mgonjwa huyo.





