Jela Miaka 30 kwa Tuhuma za Mkumbaka Shangazi
Jela Miaka 30 kwa Tuhuma za Mkumbaka Shangazi
Mahakama ya Wilaya ya Mbeya imemhukumu Reiga Innocent (21), Mchimbaji wa madini na Mkazi wa Iwindi, Mbalizi, Mkoani Mbeya, kifungo cha miaka 30 Jela baada ya kupatikana na hatia ya kumbaka Shangazi yake mwenye umri wa miaka 63.
Hukumu hiyo imetolewa na Hakimu wa Mahakama hiyo, Tedy Mrimba, Mahakama imeeleza kuwa tukio hilo lilitokea Agosti 29, 2026, majira ya jioni, wakati Mshtakiwa alipofika Nyumbani kwa mhanga na kumkuta akiwa peke yake. Kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa Mahakamani, Mshtakiwa alimshika mhanga kwa nguvu kabla ya kumbaka, tukio hilo lilisababisha kufunguliwa kwa kesi iliyomkuta Mshtakiwa na hatia ya kosa hilo.
Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Imelda Luko, ameiomba Mahakama kutoa adhabu kali kwa Mshtakiwa ili iwe fundisho kwake na kwa Watu wengine wenye tabia kama hiyo, kwa lengo la kukomesha vitendo vya ukatili katika Jami.





