Watatu Wafariki Dunia 40 Wakiokolewa Meli ikitektea kwa Moto Ziwa Nyasa

Watatu Wafariki Dunia 40 Wakiokolewa Meli ikitektea kwa Moto Ziwa Nyasa

Watu watatu, wakiwamo raia wa Msumbiji na Malawi, pamoja na Mtanzania, wamefariki dunia baada ya meli ya MV Chambo, inayofanya safari zake kati ya Tanzania na Msumbiji, kuwaka moto katika Ziwa Nyasa, mkoani Ruvuma, leo Jumapili, Oktoba 11, 2026, saa 10:30 alfajiri.

Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Nyasa, Peresi Magiri, amesema meli hiyo ilikuwa ikitoka Tanzania kuelekea Msumbiji ikiwa na tani 10 za mzigo na abiria 44 wa mataifa mbalimbali. Amesema abiria hao walikuwa raia wanne wa Malawi, 23 wa Msumbiji, 15 wa Tanzania na wawili wa Lesotho. Hi ina maana kwamba zaidi ya watu 40 waliokolewa. Ameeleza kuwa waliofariki ni mtoto wa kike, raia wa Msumbiji; mwanamke, raia wa Malawi; na Mtanzania aliyejulikana kwa jina la Yuston Chatanda, mkazi wa Njombe.

“Meli hiyo imeondoka leo, Oktoba 11, saa 10:30 alfajiri. Ajali imetokea eneo la Tanzania ikiwa na abiria 44, na watatu wamefariki dunia na wengine wameokolewa. Kazi ya kuzima moto inaendelea chini ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji,” amesema Magiri.

Amesema taratibu nyingine zinaendelea, zikiwamo mawasiliano na nchi jirani za Msumbiji na Malawi. Ameeleza kuwa Msumbiji imetuma boti ndogo kuchukua mwili wa raia wake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button