Simbu kuipeperusha bendera ya Tanzania leo Marekani
Simbu kuipeperusha bendera ya Tanzania leo Marekani
Mwanariadha wa Tanzania, Alphonce Felix Simbu leo Jumatatu, Aprili 20, 2026 anatarajiwa kuipeperusha bendera ya Taifa katika mashindano makubwa ya riadha ya Boston Marathon 2026 yanayofanyika jijini Boston nchini Marekani.
Katika mbio hizo, Simbu atatimua vumbi kilomita 42, akichuana na bingwa mtetezi, John Korir raia wa Kenya na wanariadha wengine mataifa mbalimbali duniani.
Mashindano hayo hufanyika kila mwaka yakikutanisha wanariadha wa mbio ndefu, ambapo macho yataelekezwa kwa mabingwa watetezi, John Korir kwa upande wa wanaume na Sharon Lokedi kwa wanawake, ambao wanatarajiwa kuongoza mbio hizo zenye ushindani mkali.
Tangu kuanzishwa kwake mwaka 1897, mbio hizo zimeendelea kuwa kivutio kikubwa kwa wanariadha na mashabiki wa riadha duniani kote.



